HABARI #MATUKIO || 22 wahofiwa kufa maji ziwa Tanganyika
Watu 22 wahofiwa kufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafilia kugongana na boti iliyotambulika kwa jina la Atakalo Mola, na hivyo kupasuka na kuzama.
Tukio hilo la kusikitisha lililotokea jana majira ya saa 9 usiku katika ziwa Tanganyika, limethibitiswa na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Sweetbert Njewike.
Akizingumzia tukio hilo, Kamanda Njewike amesema, mtumbwi huo ulikuwa na abilia 137 waliokuwa wakienda kwenye mkutanao wa Injiri, huku boti “Atakalo Mola” iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda Kyala ilikuwa na abilia 65.
Kati ya hao, abilia 115 wameokolewa wakati juhudi zaidi kuwatafuta wengine, zinazofanywa na polisi wakishirikiana na wananchi na jeshi la ulinzi wa wananchi zikiendelea.
Sababu zaidi kuhusiana na ajari hiyo, zimeelezwa kuwa ni pamoja na boti hizo kufanya safari za usiku, suala ambalo ni kinyume na sheria za nchi na dosari zingine kama vifaa vya uokoaji yanapotokea majanga kama haya.
Hadi sasa miili minne imeopolewa na kutambuliwa na ndugu zao.
Endelea kukaa nasi kwa taarifa zaidi.
Post a Comment