NEWS #MATUKIO || Miili sita zaidi yaopolewa ziwa Tanganyika, idadi ya waliopoteza maisha yafikia 19.


Kutoka Kigoma.

Miili ya wanakwaya walikufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafilia kugongana na boti na kisha kuzama, sasa yafikia 19 baada ya mengine sita kuopolewa.

Waumini hao wa Kanisa la Pentekoste waliokuwa wanakwenda kwenye mkutano wa Injiri katika kijiji cha Sunuka, wakitumia mtumbwi ulitajwa kwa jina la "MV Pasaka" walipatwa na maafa hayo usiku wa kuamkia ijumaa, baada ya mtumbwi wao kugongana na boti iliyotambulika kwa jina la Atakalo Mola, na hivyo kupelekea vifo vya wasafiri 19 hadi sasa.


Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili, Ofisa  Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) mkoa wa Kigoma,  Amaniel Sekulu amesema, miili sita ya watu waliozama katika hiyo, imeopolewa na hivyo kufikisha idadi ya watu 19 waliopoteza maisha hadi sasa.

Aidha ofisa huyo ameongeza kuwa, miili hiyo sita imeharibika kutokana na kukaa majini kwa muda mrefu.

Zoezi la uopoaji wa miili mingine inayofanywa na Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)  na wananchi, linaendelea licha ya kuwepo na changamoto nyingi ikiwemo kina kirefu cha maji, mawimbi makubwa na mvua zinazonyesha mara kwa mara.