TODAY'S NEWS #TANZIA || Mke wa mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru afariki dunia.



Leo Alhamisi, Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kifo cha Peras Kingunge kimetokea Leo hospitali ya taifa ya Muhimbili wakati ambao Mzee Kingunge akiwa mgonjwa hospitali hapohapo.

Akithibitisha taarifa hizo, mtoto wa Marehemu,  Kinje Ngombale amesema, "Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndiyo kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka" 

Tunatoa pole kwa familia na watanzania wote kwa msiba huo.